Thursday, April 25, 2013

Jiji la Dar es salaam

Unalionaje jiji la Dar es salaam jinsi linavyoonekana kutokea angani au ukiangalia picha zake!ni mji mzuri sana ambao ninaamini mtanzania yeyote hutamani kufika au kuishi mara anapoutizama.Lakini ni kinyume sana unapokuwa uko katikati ya jiji hili,kumebubikwa na marundo ya uchafu,michanga barabarani,mitaro iliyopasuka au kuziba maji harufu mbaya mpaka hamu ya kuendelea kukaa katika jiji hili inakuisha.Mtakubaliana na mimi usafi hapa unakosa tu usimamizi wa kutosha kwani nilifanikiwa kutembelea mji wa Moshi sikuamini macho yangu na hata wengine mtakuwa mashahidi mji ni msafi sana,hauna majengo mazuri na makubwa kama Dar es salaam lakini unavutia,ningeomba wakazi wa jiji hili tupeane mikakati nini kifanyike ili tufanikishe kuufanya mji wetu huu ili uweze kuwa na usafi ambao utafanya uwe wa kuvutia zaidi ya muonekano wa kwenye picha.
City of Dar es Salaam

No comments: